Wanaume, uwezo wako kitandani unategemea kwa asilimia 80 kile… — WANAUME CONNECT — TG.ME

Wanaume, uwezo wako kitandani unategemea kwa asilimia 80 kile unachokula kila siku - hakuna miujiza. Wanaume wengi wanakula matakataka na vyakula vya ovyo, halafu wanatarajia kuwa na nguvu za farasi dume kitandani - hiyo haiwezekani. Tilia mkazo vyakula hivi 7 na utakuwa na nguvu zaidi kitandani (Hifadhi huu ujumbe). 1. Mayai Mayai ni moja ya vyakula vyenye nguvu sana. Yamejaa protinina mafuta mazuri yanayosaidia uzalishaji wa homoni. Pia yana cholesterol, ambayo husaidia kutengeneza testosterone. Ikiwa homoni zako ziko chini, kula Mayai mwanangu. 2. Spinachi Spinachi ina magnesiamu kwa wingi, madini ambayo wanaume wengi wanakosa. Magnesiamu husaidia kulegeza mishipa ya damu na kuboresha mzunguko wa damu, jambo muhimu kabisa kutafuta heshima - Unahitaji damu ya kutosha mahali husika. 3. Samaki aina ya sangara & dagaa Wana mafuta ya omega-3 ambayo husaidia afya ya moyo na kupunguza inflammation mwilini. Moyo wako unasimamia mzunguko wa damu, na mzunguko huo unaamua jinsi mwili wako unavyofanya kazi. Kama damu haisafiri vizuri, hakuna kinachofanya kazi ipasavyo ikiwemo uume wako. 4. Mbegu za maboga Mbegu za maboga zina zinki kwa wingi, ambayo ni madini muhimu sana kwa wanaume. Zinki ina jukumu kubwa katika kusawazisha homoni na afya ya uzazi. Zinki kidogo = testosterone kidogo. 5. Ndizi Ndizi zina potasiamu nyingi, inayosaidia ishara za neva na utendaji wa misuli. Pia husaidia kudumisha nguvu na kuzuia uchovu. Kama nguvu zako zinashuka haraka, utendaji wako pia utashuka. 6. Kitunguu saumu Napenda kumeza kila siku - Kitunguu saumu kina viambato vinavyosaidia kuboresha mzunguko wa damu na kupunguza mafuta yanayoziba mishipa. 7. Parachichi Parachichi lina mafuta mazuri na vitamini E, ambavyo husaidia afya ya homoni. Kupata Mpangilio wa chakula, program zangu za kupungua, kuondoa kitambi na kupona magonjwa sugu nitumie neno COACH WhatsApp 0628908800 We Are Moving. #ommyfitness #trainerwataifa https://whatsapp.com/channel/0029VbBVv5n4Y9lf6q7gdX0l

❤2
April 22, 2026 942