tukakimbilia VPN
Lakini tulishtuka: hata data yenyewe haikuwaka kabisa.
VPN nayo ilikataa kuunganika.
Hii haikuwa “kufunga mitandao ya kijamii” kama kawaida — ilikuwa shutdown ya data kwa ngazi ya watoa huduma (ISPs).
Kwa lugha rahisi: walizima kabisa huduma ya intaneti yenyewe, si app.
Kawaida kuna njia tatu za kuzima mawasiliano:
1️⃣ Kuzuia app fulani (mfano WhatsApp pekee)
2️⃣ Kuzuia tovuti au mitandao kupitia DNS/IP
3️⃣ Kuzima huduma ya data kabisa — hakuna intaneti kabisa
Safari hii ilitumika njia ya tatu. Ndiyo maana data haikuwaka.
Sasa hivi wamefungua tena huduma ya data, lakini bado kuna vizuizi vinavyodhibiti tovuti na app fulani — ndiyo maana tunalazimika kutumia VPN ili “kupita juu” ya mfumo huo wa filtering.
📡 Kwa kifupi:
Sio kwamba VPN zilishindwa, bali hakuna intaneti ya kupita nazo.
Na sasa, intaneti ipo ila njia zimewekewa vizuizi.
Uelewa ndio nguvu ya kwanza ya uhuru. 💭 @Hora_Tech #vpn #shutdown #intarnet #app

