KWANINI HATA VPN HAIKU FANYA KAZI WAKATI MITANDAO ILIZIMWA?… — Hora Tech — TG.ME

🧠KWANINI HATA VPN HAIKU FANYA KAZI WAKATI MITANDAO ILIZIMWA? tukakimbilia VPN Lakini tulishtuka: hata data yenyewe haikuwaka kabisa. VPN nayo ilikataa kuunganika. Hii haikuwa “kufunga mitandao ya kijamii” kama kawaida — ilikuwa shutdown ya data kwa ngazi ya watoa huduma (ISPs).  Kwa lugha rahisi: walizima kabisa huduma ya intaneti yenyewe, si app. Kawaida kuna njia tatu za kuzima mawasiliano: 1️⃣ Kuzuia app fulani (mfano WhatsApp pekee)  2️⃣ Kuzuia tovuti au mitandao kupitia DNS/IP  3️⃣ Kuzima huduma ya data kabisa — hakuna intaneti kabisa  Safari hii ilitumika njia ya tatu. Ndiyo maana data haikuwaka. Sasa hivi wamefungua tena huduma ya data, lakini bado kuna vizuizi vinavyodhibiti tovuti na app fulani — ndiyo maana tunalazimika kutumia VPN ili “kupita juu” ya mfumo huo wa filtering. 📡 Kwa kifupi:  Sio kwamba VPN zilishindwa, bali hakuna intaneti ya kupita nazo.  Na sasa, intaneti ipo ila njia zimewekewa vizuizi. Uelewa ndio nguvu ya kwanza ya uhuru. 💭 @Hora_Tech #vpn #shutdown #intarnet #app

November 4, 2025 751 3 2