🇹🇿🇷🇺 Vijana wa Tanzania wajigundulia Yugra
🖥️🎤 Katika Jumba la Urusi, kulifanyika mkutano na washiriki wa programu ya "Salamu, Urusi!", ambayo ilifanyika tarehe 6 – 11 Agosti kule Yugra. Tanzania iliwakilishwa na K. Kiwale, M. Kihoro na T. Kabelwa. Katika mkutano huo, vijana hao waliwasilisha tathmini na hisia zao juu ya safari hiyo iliyokuwa imesheheni matukio mengi.
🦣🌄 Kwa siku chache hizo, wawakilishi hao walijifunza historia, mazingira na utamaduni wa HMAO. Kilichoibua msisimko mkubwa zaidi ndani yao, ni ziara waliyofanya katika Jumba la Makumbusho ya Mazingira na Binadamu, pamoja na maonyesho ya mamalia, utambulisho wa undani wa TV ya “Ugra Media Holding” na pia darasa-taaluma la Kiwanda Cha Chokoleti cha “Ethnika”.
🫂🤩 Mbali na safari, wavulana na wasichana walifanya kazi ki-timu, na kujipatia marafiki kutoka pembe zote za dunia na wakawa wamepata uzoefu muhimu wa kushiriki katika mradi huu wa kimataifa. Tunawatakia mafanikio na uvumbuzi wa mapya mengi!
5August 27, 2026 67 1









