DAR: Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetangaza kusitisha kwa muda safari za ndege za TC422 na TC423 kati ya Dar es Salaam na Moscow kuanzia Septemba 4, 2026, kufuatia tathmini ya vihatarishi vya mazingira ya uendeshwaji. Abiria waliokata tiketi watapewa fursa ya kurudishiwa fedha zao au kubadilishiwa tarehe au njia mbadala.
Ikumbukwe, Juni 05, 2026, akizungumza katika Jukwaa la 29 la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF 2026) nchini Urusi, Rais Samia alisema safari ya Dar na Moscow zitaanza Julai 2, 2026 ikiwa ni hatua ya kuimarisha biashara, uwekezaji na utalii kati ya Tanzania na Urusi.
Zaidi https://jamii.app/AtclSafariMoscow
#JamiiForums #JFEconomy #JFDiplomacy

1September 4, 2026 44